Powered By Blogger

Sunday, July 29, 2012

Sababu Za Kukosa Usingizi:

Tatizo la kukosa usingizi (insomnia) ni matatizo ya kawaida sana kwa watu wengi. Japokuwa tatizo ili utofautiana kutoka mtu hadi mtu, lakini watu wengi sana wanasindwa kuelewa kuwa tatizo la kukosa usingizi ni dalili ya matatizo ambayo yamejificha na hayaja jitokeza bado. Kwa ufupi ukosefu wa usingizi ni dalili ya tatizo jingine. Wakati mwingine usababishwa na unywaji wa vimiminika vyenye caffeine kwa wingi au kwa uchache au unywaji wa pombe na haswa wakati wa mchana au wakati mwingine ni kutokana na mambo yanayo kusumbuwa kifikra au matumizi ya madawa ya kitabibu au mambo ambayo yamekuwa mengi kichwani kiasi una kuwa overloaded na majukumu yako aidha kikazi au nyumbani au kifamilia.

Ili kujua jinsi gani unaweza kutibu tatizo lako, kuna mambo kadhaa ambayo unapaswa kuyaelewa kwanza, kabla ya kuvamia madawa ya kukupa usingizi.

Ili kutatua tatizo lako la kukosa usingizi unapaswa kuzingatia sana jinsi ya style yako ya kimaisha na unautumiaje mchana wako, je ukusababishia mawazo baadae haswa nyakati za usiku? Hapa namaanisha mazingira yako ya kila siku, je yana kusababishia maudhi na kero? Kwa sababu vitu vidogo vidogo kama hivi, au kuogopa kukutana na watu kunaweza kukupelekea ukakosa usingizi wakati wa usiku.

· Je, kuna jambo linalokupa dhiki ya moyo? (Kama vile stress?)
· Je, unasumbuliwa na unyogofu au huzuni (are you depressed?)
· Je, una hisia za wasiwasi au hofu kwa muda mrefu?
· Je, unatumia dawa zozote ambazo zinaweza kuathiri usingizi wako?
· Je, una matatizo yoyote ya kiafya ambayo zinaweza kuathiri usingizi wako?
· Je, eneo unalotumia usiku kulala lipo katika mazingira ya utulivu na starehe?
· Je unatumia muda wa kutosha kupata mwanga wa jua wakati wa mchana na usiku unalala kwenye kiza cha kutosha au unaogopa kiza?

Matatizo Ya Kisaikolojia Ambayo Yanaweza Kusababisha Kutopata Usingizi:

Unyogovu (depression), wasiwasi (anxiety), msongo wa muda mrefu (stress), bipolar disorder (Tatizo la kwenye ubongo). Woga wa kukutana na watu, au kukikosa kile unacho kipenda au kukitarajia kwa muda mrefu, na kutumia sana kompyuta.

Madawa Ambayo Yanaweza Kusababisha Kukosa Usingizi:
Antidepressants, dawa za mafua kama vile dawa za flu, madawa ambayo yana kilevi (alcohol) dawa za kupunguza maumivu zenye caffeine, dawa za homoni, madawa ya shinikizo la damu.
Haya utokea kama umekuwa ukiyatumia kwa muda mrefu au hata kwa muda mfupi, inategemea na mwili wako.

Matatizo Ya Kiafya Ambayo Yanayoweza Kusababisha Kukosa Usingizi:
Pumu (asthma), allergy (Mzio) ugonjwa wa Parkinson, hyperthyroidism, acid reflux, ugonjwa wa figo, saratani, au maumivu ya muda mrefu.

Vitu Vidogo Vidogo Ambavyo Vinaweza Kusababisha Kukosa Usingizi:
Matatizo ya kutotulia wakati wa kulala, woga, kushiba sana, njaa na kutokuwa na utulivu, mawazo na wasiwasi, ugomvi ndani ya nyumba, gubu, kutohisi kujaliwa na mweza, majirani wsio kupenda au kuwapenda, kutokinahi na unacho kipata, matarajio yasiowezwa kufikiwa, kukikosa kile ambacho ukikitarajia kukipata, kujali sana matatizo ya wenzako na kuhisi wewe umechangia kukosa kwao, au unahisi wewe una wajibu wa kuwasaidia na uwezo huna, wivu, kutamani usichoweza kukipata.

Njia Za Kusaidia Kupata Usingizi:
Kama unakosa usingizi, haya yafuatayo yakizingatiwa yanaweza kusaidia kurudisha hali ya kupata usingizi wa kawaida.

  • Jambo la kwanza ondoa mawazo ya kutopata usingizi. Epuka kuwa na wasiwasi, woga na acha kufikiria matatizo yako uliokumbana nayo mchana kutwa, kama vile maudhi n.k, usishibe sana, wala kulala na njaa,
  • Ondoa mawazo na wasiwasi,
  • Kitanda chako kiwe ni sehemu ya kulala, na si chumba cha kutazama TV/video
  • Chumba kiwe ni sehemu ya kulala na faragha za kichumbani, chumba kisitumiwe kwa ajili ya kufanya kazi za ofisini, kusoma, kuangalia Luninga, au kutumia kompyuta (laptop, ipad simu na vinavyo fanana na hivyo) kitandani.
  • Jaribu kuwa na mausiano mazuri na kukipa haki yake chumba, chumba cha kulala ni sehemu pekee ambapo ubongo wako na mwili wako utapata utulivu, hii itapeleka meseji kwenye ubongo na kusababishia utulivu na kukupatia usingizi.
  • Kumbuka kwamba matatizo ya kimaisha hayaishi na hayatatuliwi kwa siku moja, kwa hiyo usilazimishe kuyatatua kwa kuyafikiria wakati wa usiku. Wakti wa usiku ni wakati wa kulala tu. Q 28: 71-73
  • Kama utakosa usingizi, usichukie, pokea hiyo taarifa kama unavyopokea taarifa nzuri. Nyanyuka kitandani, usilazimishe kulala, kwani kitendo cha kulazimisha kulala kitakupelekea kuwa na wasiwasi na kukuchosha na wakati mwingine kukusababishia hasira kwa sababu ya kukosa usingizi.
  • Amka, nenda ukumbini au varandani ili kubadilisha mazingira, fanya jambo lolote ambalo litakupa kazi ila isiwe ya kukuchosha, kama vile kunyayua vitu vizito au kuanza kufua n.k, unaweza kuchukuwa tafasiri ya Qur’an na kusoma au kufanya Tasbiih, Tahmiid, Tahliil, au kusikiliza kanda za mawaidha, uku unakunywa kinywaji chochote cha moto kisicho na caffeine,kama vile maziwa, au unaweza kutawadha (kuchukuwa udhu) au kuoga, ukasali na kuomba duwa kwa mambo mbalimbali yanayokukabili kimaisha.

Matatizo Ya Kijamii.
  • Kama kuna tatizo wewe na mwenzi wako (ugomvi ndani ya nyumba) au mtu wako wa karibi basi jaribu kuongea naye ili kuondoa tatizo kati yenu. Kusamehe wale walio kukosea ni jambo zuri sana, kwani kutakupa afueni na kukuletea raha kila unapomuona mgomvi wako.
  • Binadamu sote tuna matatizo, kuna ambayo yapo ndani ya uwezo wetu na kuna ambayo yapo nje ya uwezo wetu, usilazimishe kutatua kila tatizo la ndugu, jamaa na marafiki, maana wewe si Mungu wa kumpatia liziki kila mja/mtu.
  • Tosheka na unacho kipata au kupewa, usilazimishe kila jambo liwe high quality. Mengine wacha yakupite, na si kila fasheni ni lazima uwe nayo sahau matarajio yasiowezwa kufikiwa.
  • Kumbuka kuwa kama kuna ndugu au marafiki ambao hawaonyeshi kukujali, basi kuna ambao wanakujali ila hawajapata nafasi ya kukwambia kuwa wanakujali, wakati mwingine wanaogopa tu kukwambia kwa sababu umesha weka distance nao na kujiona wewe kuwa ni matawi ya juu, na hakuna wa kukufikia. Jaribu kuwa karibu sana na watu haswa ndugu, jamaa na marafiki. Maisha ya uzungu kwa wanaoishi Afrika hayafai, yanasababisha matatizo na kutengwa.

Kabla Ya Kufikiria Kutafuta Mtaalamu Wa Tiba Ya Usingizi Zingatia Yafuatayo

• Muone mtaalamu, ikiwa kukosa kwako usingizi kunaathiri utendaji wako wa kazi ofisini, kazini au shuleni.
• Kama kukosa kwako usingizi kunakupelekea kuwa na hasira, woga na wasiwasi na kama unaanza kupata fikra mbaya dhidi yako binafsi au watu wanao kuzunguka, haswa watu wa karibu na wewe, au unahisi watu wanakuchukia na kukusema, au kama unaanza kusikia sauti ya mtu au watu wanakusemesha.
• Kama unahisi maumivu ya kifua, au uvutaji wakoo wa pumzi unaleta matatizo.
• Vile vile kama ili ni tatizo la muda mrefu, basi inashauriwa kumuona mtaalam aliyebobea kwenye masuala ya insomnia ili kupata maelekezo yake ya kitaalam.
• Kumbuka kuwa hakuna jambo dogo kwenye maisha ya binadamu, lile ambalo unaliona dogo, lakini linaweza kuwa ndio chanzo cha wewe kukosa usingizi, wakati mwingine hata kuto ambiwa ahsante na mumeo, mkeo, ndugu au rafiki wa karibu, kunaweza kusababisha matatizo ya kisaikolojia na kujiona kuwa huna thamani na kila unalolifanya alithaminiwi na wale unao amini kuwa ni vipenzi vyako.


Unaweza ku google kuhusiana na matatizo ya kukosa usingizi;
Website:
Can't Sleep? 15 Proven Tips for Insomnia
http://www.selfhelpmagazine.com/article/insomnia

Why can't I get to sleep?
http://www.independent.ie/health/health-advice/why-cant-i-get-to-sleep-1343565.html

Can’t Sleep?
INSOMNIA CAUSES, CURES, AND TREATMENTS

http://www.helpguide.org/life/insomnia_treatment.htm

No comments:

Post a Comment